JANETH KALINGA & SAMSON MANYALA 
sayansi ya kumzaa mtoto mwerevu [EPUB ebook] 

Supporto

Kim Ung-yong alizaliwa nchini Korea ya Kusini katika jiji la Seoul. Alipokuwa na umri wa mwaka mmoja tu, tayari alikuwa amejifunza alphabeti za Kikorea na maumbo (characters) 1, 000 ya lugha ya Kichina. Alipofikisha umri wa miaka mitatu alikuwa anaweza kufanya hisabati ngumu za mada ya 'calculus'. Kim alipofikisha umri wa miaka mitano, tayari alikuwa ametunga, kuchapisha na kuuza kitabu chake cha kwanza. Ni katika umri huo wa miaka mitano Kim alikuwa akiongea vizuri lugha za Kikorea, Kijapani, kingereza, Kifaransa na Kijerumani! Kitabu hiki kimesheheni mifano ya watoto waliozaliwa na akili za juu kama Kim. Hawa ni watoto ambao kila mzazi angetamani kuwanao. Ni kweli kwamba, sababu za vinasaba 'genetic' zaweza kuwa moja ya vyanzo vya mtoto kuzaliwa na akili za juu kuliko kawaida (more than 100% of IQ), lakini tafiti za kisayansi zinamletea mzazi kanuni nyepesi za kumwezesha kumzaa mtoto mwerevu .
Ni dhahiri kwamba, haiwezekani kubadilisha vinasaba vilivyomo katika seli za baba au mama ili apatikane mtoto mwenye akili za juu za kipekee, lakini, wenza wawili wanayo nafasi ya kuchaguana kwa kujali ubora wa mbegu za kiume na ubora wa mayai kwa jinsia ya kike: Hapo swala la umri wa wenza; uwiano wa umri baina yao; na katika umri upi wapate mtoto na umri upi wasizae kabisa ni mambo ya msingi . Hilo limeongelewa kwa mapana. kitabu pia kinamuongoza mzazi katika kanuni za kuboresha homoni 'hormones' zinazohusiana na ujenzi wa ubongo na akili kwa ujumla. Kitabu kinaaza na homoni za mama na kisha homoni za mtoto mwenyewe. Aidha, kitabu kinaelezea namna ya kutengeneza mazingira ya mtoto kuanzia mazingira ya tumboni mwa mama na mazingira ya baada ya kuzaliwa. Kanuni hizo na zingine kadhaa ndizo mada zilizomo katika kitabu hiki. Ni bayana kwamba kwa kiwango kikubwa, ukosefu wa maarifa, uzembe na umaskini ndivyo vimewasababishia watoto wengi udumavu wa akili.
SAYANSI YA KUMZAA MTOTO MWEREVU ni kitabu kinachomfundisha mzazi namna ya kumzaa (kumpata) mtoto ambaye kama hatafikia kiwango cha kuitwa "prodigy" au "genius", basi ataitwa mwerevu ; yaani binadamu mwenye uwezo mzuri katika kuyamudu masomo yake na kutatua changamoto za maisha. Elimu hii, inamuandaa mtoto kuanzia mazingira ya kabla ya kutungwa kwa mimba yake; kichanga tumboni; kuzaliwa na kufikisha umri wa miaka minne.
Mtoto aliyeandaliwa kwa sayansi hii, daima atakuwa ni mshindi masomoni na maishani. Kitabu hiki, ni mkusanyiko wa tafiti zilizofanywa na wataalamu mahiri wa mambo ya afya, saikolojia, elimu, sanaa na wengineo katika mabara ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Ulaya, Asia na Australia. Baadhi ya tafiti hizi zimechukua takriban muda wa miaka 40 ili kukamilika!
Msomaji atagundua kwamba, kabla hajafanya uamuzi wa kuzaa na mwenza wa namna gani, alipaswa kwanza kupata maarifa yaliyoko humu. Lakini pia, kama tayari uchaguzi wake haukuwa wa kisayansi katika kumchagua mwenza, basi bado yapo maarifa ya kurekebisha dosari za kumzuia kumpata mtoto mwerevu. Kitabu chafaa kabla ya ujauzito, na kama mzazi amechelewa kupata maarifa haya, basi elimu hii bado itafaa endapo mtoto hajafikisha umri wa miaka minne. Hilo ni angalizo muhimu lenye sababu za kibaiolojia.
Bi. Janeth Kalinga ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (DUCE) pamoja na mwandishi mahiri wa vitabu Mwl. Samson Manyala , wamekuandalia kitabu hiki katika lugha rahisi kueleweka. Aidha, japo mtoto na mzazi aliyeongelewa ni wakitanzania, lakini kitabu bado kinabakia kuwa ufumbuzi kwa wazazi wote wanaoelewa au kutumia lugha ya Kiswahili kokote ulimwenguni. Kama ilivyo kwa Tanzania, kitabu hiki ni muhafaka vilevile kwa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, na Malawi. Nchi hizi licha ya kuwa watumiaji au waelewa wa Kiswahili, lakini mazingira yao na changamoto zao kijamii (kielimu) na kiuchumi hazitofautiani sana na za Tanzania.

€2.99
Modalità di pagamento
Acquista questo ebook e ricevine 1 in più GRATIS!
Formato EPUB ● ISBN 9788835372110 ● Dimensione 2.1 MB ● Casa editrice SAMSON JOSEPHAT MANYALA ● Pubblicato 2020 ● Scaricabile 24 mesi ● Moneta EUR ● ID 7381630 ● Protezione dalla copia senza

Altri ebook dello stesso autore / Editore

22.437 Ebook in questa categoria