Walinzi Wa Lango La Hekalu
Tathimini Ya Mchango Wa Mlinda Lango Katika Hekalula Agano La Kale Na Mafundisho Yake Kwenye Maisha Ya Ukristo Leo
Mara nyingi bila kutambuliwa, walinzi wa Agano la Kale walilinda hekalu kutokana na kitu chochote kichafu, wakisimamia mambo ya kifedha kwa uaminifu na kudumisha mali ya hekalu. Walikuwa sehemu muhimu ya ibada ya Agano la Kale, wakihakikisha kwamba Bwana Mungu wao aliheshimiwa na kuheshimiwa katika mahali palipotengwa kwa ajili ya jina Lake.
Wanaume hawa wa imani hutufundisha mengi kuhusu Mungu na kile anachohitaji. Katika enzi ambapo mivuto ya ulimwengu inakubalika zaidi na zaidi katika kanisa, tungefanya vyema kuwasikiliza walinzi wa malango wa siku zetu kwa makini.
Spis treści
Dibaji
Sura ya 1 – Walinzi
Sura ya 2 – Kulinda Mlango
Sura ya 3 – Kulinda Mali ya Hekalu
Sura ya 4 – Fedha za Hekalu
Sura ya 5 – Walinda Lango na Ibada ya Yehova
Sura ya 6 – Nafasi ya Heshima
Sura ya 7 – Picha ya Kazi ya Bwana
Sura ya 8 – Masomo ya Kujifunza Kutoka kwa Walinda Lango la Hekalu
O autorze
F. Wayne Mac Leod alizaliwa Sydney Mines, Nova Scotia, Canada na alikasoma Ontario Bible College, Chuo kikuu cha Waterloo na Ontario Theological Seminary. Aliwekewa mikono katika kanisa la Baptist Hespeler huko Cambridge, Ontario Mwaka 1991. Yeye na Mke wake Diana walitumika kama Wamishenari na shirika lililoitwa Africa Evangelical Fellowship katika Visiwa vya Mauritania na Reunion katika bahari ya hindi tangu mwaka 1985 – 1993 ambapo Wayne alikuwa anafanyakazi ya Maendeleo ya kanisa na kufundisha Viongozi. Kwa sasa anafanya huduma ya uandishi wa Vitabu na ni Mwanachana wa Action International Ministries.