Hili ni fundisho la Luka 15:3-7. Katika njia nyingi fumbo hili linahusu namna ya kuwa Mchungaji mwaminifu wa Kondoo wa Mungu.
Inafunua moyo wa Bwana Yesu kwa watu wake wa Thamani ambao wamepotea nji. Ni wito kwa wote ambao watasikia mafundisho yake kuusikia moyo wa Mungu kwa ajili ya wale mbao ushirika wao na furaha vimezuiliwa. Huduma ya kurejesha kondoo kwenye ushirika si kazi rahisi. Ni kwa mtu ambae, anapendezwa na moyo wa Mungu. Nina shawishika kuwa utajri wa Baraka zake zitakaa juu ya wale wanaoshiriki kujali kwake kwa ajili ya Kondoo waliokwenda mbali.
Giới thiệu về tác giả
F. Wayne Mac Leod alizaliwa Sydney Mines, Nova Scotia, Canada na alikasoma Ontario Bible College, Chuo kikuu cha Waterloo na Ontario Theological Seminary. Aliwekewa mikono katika kanisa la Baptist Hespeler huko Cambridge, Ontario Mwaka 1991. Yeye na Mke wake Diana walitumika kama Wamishenari na shirika lililoitwa Africa Evangelical Fellowship katika Visiwa vya Mauritania na Reunion katika bahari ya hindi tangu mwaka 1985 – 1993 ambapo Wayne alikuwa anafanyakazi ya Maendeleo ya kanisa na kufundisha Viongozi. Kwa sasa anafanya huduma ya uandishi wa Vitabu na ni Mwanachana wa Action International Ministries.