Nabii Wa Moto Na Watu Waliogeuka Kuni
Nabii wa moto, hivyo ndivyo Yeremia alivyokuwa. Ujumbe wake ulichoma wale waliomsikia akisema. Hakuna mtu anayependa kuchomwa moto. Kwa sababu hiyo, wasikilizaji wake walitaka kumuua. Wakamtupa gerezani. Hakuwa na marafiki wengi. Hakuwahi kuoa na hakuwa na watoto wa kuendeleza jina lake. Kwa miaka arobaini, hata hivyo, alitangaza neno la Bwana kwa uaminifu kwa watu ambao waligeuza migongo yao na kuziba masikio yao. Yeye ni mfano wa ibada ya kweli na uvumilivu. Utafiti huu unachunguza matukio muhimu na jumbe za mtu huyu mkuu wa Mungu.
Inhoudsopgave
DIBAJI
SURA YA 1 – SARAFU YA MJANE
SURA YA 2 – KUITWA KABLA YA KUZALIWA
SURA YA 3 – MIMI NI MTOTO TU
SURA YA 4 – ISHARA MBILI
SURA YA 5 – MANENO YA MOTO MIONGONI MWA WATU WALIOGEUKA KUNI
SURA YA 6 – HEKALU LA BWANA
SURA YA 7 – MAPIGO HALISI
SURA YA 8- MKANDA ULIOHARIBIKA
SURA YA 9- USIWAOMBEE WATU HAWA
SURA YA 10 – NABII MPWEKE
SURA YA 11- KWENYE NYUMBA YA MFINYANZI
SURA YA 12 – MTUNGI WA UDONGO ULIOVUNJIKA
SURA YA 13 SEDEKIA NA YEREMIA
SURA YA 14 WACHUNGAJI WASIOJALI NA MANABII WA UONGO
SURA YA 15 – NJAMA YA KUMUUA YEREMIA
SURA YA 16 – JUMBE ZINAZOKINZANA
SURA YA 17 – NYUMBA YA SHAFANI
SURA YA 18 – TAFUTA AMANI YA JIJI
SURA YA 19 – NIDHAMU YA BWANA
SURA YA 20- TENDA KILE UNACHOHUBIRI
SURA YA 21 – WATUMWA WALIORUDISHWA
SURA YA 22 – WAREKABI
SURA YA 23 – GOMBO LILILOCHOMWA
SURA YA 24 -UOGA JUU YA MAISHA YAKE
SURA YA 25 – KURUDI MISRI
SURA YA 26 – ZAMA WALA HAUTAZUKA TENA
Over de auteur
F. Wayne Mac Leod alizaliwa Sydney Mines, Nova Scotia, Canada na alikasoma Ontario Bible College, Chuo kikuu cha Waterloo na Ontario Theological Seminary. Aliwekewa mikono katika kanisa la Baptist Hespeler huko Cambridge, Ontario Mwaka 1991. Yeye na Mke wake Diana walitumika kama Wamishenari na shirika lililoitwa Africa Evangelical Fellowship katika Visiwa vya Mauritania na Reunion katika bahari ya hindi tangu mwaka 1985 – 1993 ambapo Wayne alikuwa anafanyakazi ya Maendeleo ya kanisa na kufundisha Viongozi. Kwa sasa anafanya huduma ya uandishi wa Vitabu na ni Mwanachana wa Action International Ministries.